Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a) – ABNA –, Guy Pearce, mwigizaji mashuhuri wa Australia, amelaani vikali utawala wa Kizayuni kutokana na “kutojali kabisa maisha ya Wapalestina” wakati wa mashambulizi yanayoendelea dhidi ya Gaza na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Katika chapisho aliloweka siku ya Jumapili kwenye mtandao wa kijamii X (zamani Twitter), Pearce aliandika: “Sijawahi katika maisha yangu kuchukizwa na kikundi cha watu kama ninavyokerwa na kitendo cha Waisraeli.”
Amesema kuwa “kila siku nashuhudia dharau na kutojali maisha ya Wapalestina kwa upande wa Waisraeli,” akieleza kuwa mwenendo huo ni “wa aibu” na kwamba wale wanaotekeleza “matendo haya mabaya” wanairudisha nyuma ubinadamu kila siku.
Pearce pia alishiriki kipande cha video kutoka kituo cha Al Jazeera kilichomuonyesha mvulana wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 15 akifyatuliwa risasi na wanajeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kijana huyo aliachwa bila kupatiwa huduma yoyote ya matibabu baada ya kujeruhiwa, jambo lililochangia kufariki kwake.
Your Comment